Idara ya Usafi na Mazingira ina vitengo viwili; Kitengo cha usafi na kitengo cha Mazingira. Kitengo cha Usafi kina majukumu ya kusimamia usafishaji wa mji, ukaguzi wa majengo ya vyakula maeneo ya wazi, mifereji na barabara, utunzaji, uchambuzi na usafirishaji wa taka na kusimamia uendeshaji wa vizimba vya taka. Kitengo cha Mazingira kina majukumu ya kudhibiti uchafuzi na uharibifu wa mazingira (ardhi, vyanzo vya maji,uchafuzi wa mazingira), utunzaji wa mazingirana upandaji miti, majani na maua na kufanya tathmini ya athari za mazingira katika miradi ya maendeleo.