Shirika la “Wote Sawa” linaloshughulikia Haki za wafanyakazi wa Majumbani na Usafirishaji Haramu wa Binadamu lililopo Kasulu Mjini kwakushirikiana na Shirika la Usafirishaji wakimbizi Duniani (IOM).
Mashirika haya yote yamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kupinga ukatili wa kijinsia kupitia chini ya Mpango wa Pamoja wa Kigoma Joint Program (KJP) dhidi ya Mpango wa Serikali wa kupinga Ukatili dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia pamoja na kupambana na Usafirishaji haramu wa Binadamu.
Maneja wa Shirika la Wote Sawa BI.Jackline Ngalo alisema kuwa kwa kushirikiana na Shirika la Usafirishaji wakimbizi duniani (IOM) chini ya Mpango wa “Kigoma Joint Program” wameweza kuwahudhumia wananchi 77 kuanzia mwaka 2017 hadi kufikia mwaka huu 2019, walioletwa kupitia ofisi ya ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji-Kasulu.
Wananchi waliopokelewa katika shirika la Wote sawa ni wale waliofanyiwa ukatili wa kijinsia na wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wa kike wachache wakibakia kuwa wakiume. Bi.Jackline alisema pindi waanga hao dhidi ya ukatili wa kijinsia wanapokuwepo kituoni hapo upatiwa stadi mbalimbali za maisha kama kujifunza ufundi cherehani ili wakiondoka katika kituo hicho waweze kuwa na ujuzi wa kupambana na maisha.
Pia Bw.Godfrey Kapaya Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Mji-Kasulu, aliijulisha timu hiyo kuwa, waanga hao wanapokuwepo kituoni hapo mbali na huduma wanazopatiwa wakiwepo kituoni pia upatiwa matibabu,Kuhudhuria mashauri mbalimbali mahakamani dhidi ya kesi za ukatili wa kijinsia, Elimu ya ushauri Nasaha na Baadae kuwasafirisha kwenda kuungana na familia zao.
Yote haya yamebainika kupitia ziara ya waandishi wa Habari kutoka katika Mradi KJP iliyofanyika Agosti 7,2019, Miradi inayofadhiliwa na KJP imelenga kuisaidia Jamii ya Kasulu ikiwa ni Mpango wa mashirika ya umoja wa mataifa dhidi ya maeneo yaliyoathirika na uwepo wa kambi za wakimbizi kutoka nchi za Burundi na Congo.
Kasulu Town Council
Postal Address: P.O.BOX 475
Telephone: 028-2810335
Mobile: 0784997037
Email: td@kasulutc.go.tz