Idara ya Maendeleo ya Jamii imeendesha mafunzo elekezi kwa maafisa Maendeleo kutoka Halmashauri zilizopo mkoa wa Kigoma ili kuweza kuwajengea uwezo katika kusaidia vikundi vya akinamama na vijana vilivyopo ndani ya mkoa wa kigoma.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na UN-WOMEN yamefanyika katika ukumbi wa High Way Hotel kuanzia tarehe 13 hadi 14 Juni 2019, iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Mgeni rasmi katika hotuba ya ufunguzi alisema imefika wakati wa kuvisaidia vikundi vya wanawake na vijana ili kuweza kuweka malengo ya kiuchumi.
Pia amewataka viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na mashirika mbalimbali kuunga juhudi mbalimbali za serikali katika kuwaletea wanawake na vijana maendeleo kama wanavyofanya UN-WOMEN walivyojikita kumletea mwanamke maendeleo aliyepo ndani ya mkoa wa kigoma.
Hata hivyo ilielezwa kuwa katika Hatua mbalimbali za ufuatiliaji wa fedha zinazotolewa na mamlaka na serikali za mitaa dhidi ya vikundi vya wanawake na vijana,baada ya ziara ya tathimini kufanyika, imebainika kuwa fedha nyingi zinazorejeshwa hazitumiki kukopeshwa vikundi vingine kama ilivyo kwenye muongozo.
Pia imebainika kuwa kiasi cha fedha kinachotengwa na mamlaka za mitaa kama asilimia 10 ya makusanyo yote ya mapato ya ndani kwa kila Halmashauri hakitumiki kukopesha vikundi vya wanawake na Vijana kama ilivyoainishwa kwenye miongozo mbalimbali ya serikali.
Mbali na changamoto mbalimbali zilizobainika kwenye utafiti uliofanyika, imebainika kuwa Halmashauri ya Mji wa Kasulu imefanya vizuri katika suala zima la ukopeshaji wa Fedha kwa vikundi vya akinamama na Vijana, Jambo ambalo hadi kufikia mwezi Juni 2019, ilikuwa imekopesha kwa asilimia 100 ya bajeti yake ya mapato ya ndani.
Pia wadau wameshauri kuwa taarifa mbalimbali za vikundi vilivyopatiwa mikopo ziwe pia zinapelekwa kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya.
Kasulu Town Council
Postal Address: P.O.BOX 475
Telephone: 028-2810335
Mobile: 0784997037
Email: td@kasulutc.go.tz