Wafanyabiashara katika soko la Mwilamvya waendelea kuchukua tahadhari ya kujinga na Ugonjwa COVID 19.
Haya yamebainishwa na Bi.Yabesi Lenikadi ambaye ni mfanyabiashara katika soko la Mwilamvya wa mbogamboga na Nyanya lilipo Halmashauri ya Mji wa Kasulu, wakati wa ziara ya Tathimini iliyofanywa na Wataalam kutoka shirika la IOM pamoja na Ofisi ya Mgaga Mkuu kutoka Idara ya Afya kasulu Mji.
Mbali ya uwepo wa mafanikio makubwa kuhusu kuchukua tahadhali ya ugonjwa wa CORONA kwa wafanyabiashara na wananchi wa Kasulu Mji,ikiwemo kila mfanyabiashara kunawa mikono vizuri kwenye ndoo kubwa zilizowekwa kwenye milango 4 ya kuingia kwenye soko la Mwilamvya.
Pia kuna changamoto chache ambazo zimebainika wakati wa ziara hiyo, iliyofanyika tarehe 21 mei,2020 ikiwemo baadhi ya wafanyabiashara kushidwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya ambayo wamepatiwa na timu hiyo ya Wataalam hao .Changamoto hizo ni ukosefu wa ndoo tiririsha maji pamoja na uwepo wa sabuni ya kunawa pindi mteja anapotaka kupokea huduma.
Bi.Yabesi amesema mbali na uwepo wa changamoto hiyo pia kuna changamoto ya wateja wenyewe kukataa kunawa mikono kabla ya kupokea huduma, sababu ambayo inamvunja moyo dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Corona na kushauri kuwa ni vizuri mamlaka husika zikaendelea na kutoa Elimu ili kuweza kuwakinga na Ugonjwa wa COVID 19.
Kasulu Town Council
Postal Address: P.O.BOX 475
Telephone: 028-2810335
Mobile: 0784997037
Email: td@kasulutc.go.tz