Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col.Anage amewataka viongozi wa Dini kuzingatia sheria na Taratibu za nchi katika suala zima la utoaji wa huduma za kidini,ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kupitia kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji-Kasulu, tarehe 12 Novemba 2019, ilijulishwa kuwa kuna baadhi ya makanisa yaliyopo ndani ya Mji-Kasulu yameendelea kuwa na utaratibu usiozingatia sheria na kanuni za nchi katika suala zima la utoaji huduma za kidini kwani viongozi hao wamekuwa wakipinga kelele kuanzia saa 10 alfari kila siku kwa kisingizio cha kuita waumini wao kupitia vipaza sauti vilivyofungwa nje ya makanisa na misikiti. Hivyo amewataka waheshimiwa Madiwani kwenda katika kata zao na kueleza kuwa sheria na kanuni zizingatiwe ili kuweza kuendelea kuondoa usumbufu kwa baadhi ya Wananchi ambao kwa muda huo awataki kusikia au kupigiwa kelele kupitia kwenye vipaza sauti hivyo kwani wapo wenye dini na wasiokuwa na Dini. Hivyo kiongozi yoyote ambaye atakiuka agizo hili vyombo vya ulinzi na usalama vitamchukulia sheria ikiwemo kupigwa faini.
Kasulu Town Council
Postal Address: P.O.BOX 475
Telephone: 028-2810335
Mobile: 0784997037
Email: td@kasulutc.go.tz