Idara ya Elimu Sekondari inasimamia shughuli za maendeleo katika Shule 25 za Sekondari, kati ya shule hizo, 11 ni za Serikali na 14 ni shule zisizo za serikali. Idara ina jumla ya walimu 299, Fundi sanifu Maabara 1 na maafisa 4. Kazi kubwa ya Idara ya Elimu ni kusimamia ubora wa elimu itolewayo na shule za sekondari pamoja na zile za binafsi.