Idara ya Maji iliendelea kusimamia ujenzi wa miradi ya maji Kimobwa,Heru juu na Muhunga. Utekelezaji wa miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali ambapo mradi wa maji Heru juu umekamilika kwa 75%, Mradi wa Maji kimobwa umekamilika kwa 79% na Mradi wa maji Muhunga umekamilika kwa 70%. Wakazi katika miradi ya maeneo yote matatu wameanza kunufaika na huduma ya maji kupitia miradi hiyo.Hata hivyo miradi hiyo ilitarajia kukamilika tarehe 09/03/2018 .
Idara ya Maji inaendelea na zoezi la kuunda na kusajili vyombo vya Watumia maji. Vyombo vya watumia Maji vimeundwa katika maeneo ya Kanazi, Ruhita, Heru juu, Mwanga B, Nyumbigwa, Kabanga na Msambara. Utaratibu wa kuvisajili umekamilika kwa maeneo ya kabanga na Msambara.