akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philipo Isodor Mpango ameipongeza Wizara ya Elmu, Sayansi na Teknolojia kwa Juhudi mbalimbali inazozifanya ili kuhakikisha inaboesha Miundombinu ya Elimu hapa Nchini.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Makamu wa Rais iliyofanyika Halmashauri ya Mji-Kasulu leo 17 July 2021, katika ziara hiyo Makamu ameweza kutembelea mradi wa Ujenzi wa Chuo kipya cha Ualimu Kabanga na kuweka jiwe la Msingi , ambapo mradi huo umetekelezwa kwa hisani ya watu wa Canada na umegharimu kiasi cha Dola milioni 53 za Kimarekan..
Wakati wa utekelezaji wa Mradi huo kumezingatiwa haki za wanawake na usawa wa kijinsia ili kuweza kuleta maendeleo ya wanawake nchini kwa kuwapatia haki sawa kwenye fursa za kielimu. Makamu amewataka wachuo cha ualimu kabanga kutunza Miundombinu mbalimbali iliyopo katika chuo hicho ili kuweza kutumika kwa kipindi kirefu na kuwa kujengwa upya kwa chuo hicho ni mkakati wa kuendelea kuboresha Mazingira ya Mafunzo ya Walimu Nchini ili kupata walimu wen ye maadili mema.