Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma,Mhe. Kanali Isaac Mwakisu ametoa wito kwa viongozi wa dini kuungana katika kuliombea taifa letu wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Kanali Mwakisu ameyasema hayo jana Ijumaa Machi 28,2025 wilayani humo wakati wa hafla ya futari aliyoianda kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu pamoja na wenzao wale wa Kasulu Mji.
“Serikali tumejipanga vizuri kwenye usalama,lakini tunahitaji maombi yenu ili uchaguzi huu uwe na amani,” amesema.
Aidha, Kanali Mwakisu amewakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpiga kura ambapo mchakato wake utaanza tena hivi karibuni wilayani humo.
Pia,ametoa wito kwa wananchi kujiwekea akiba ya chakula kwa kutouza mazao yote kutokana na mwenendo wa mvua mwaka huu kutokuwa wa kuridhisha.
Katika hafla hiyo,Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Masoud Kikoba amesisistiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kugombea nafasi mbalimbaliza uongozi wakati wa uchaguzi.Kwakuwa ni haki ya kila Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa kiongozi anayewakilisha matakwa yao.