SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI HALMASHAURI YA MJI KASULU KUNUFAIKA NA MADAWATI KUTOKA MFUKO WA JIMBO.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kasulu mjini Mkoani Kigoma amekabidhi madawati 722 kwa halmashauri ya Mji kasulu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini kwa mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji.
Akikabidhi madawati hayo Mbunge wa jimbo hilo Prof. Joyce Ndalichako amefafanua kua madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 59,980,00 ambayo yatasaidia kuboresha mazingira yakujifunzia ambapo amempongeza Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha njia sekta ya elimu.
Prof. Ndalichako amewasisitiza walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo ikiwa ni pamoja na kuonyesha nidhamu nzuri shuleni pia amesisitiza kuendelea kutumia fedha za jimbo kwa maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Anthony Mwakisu amemshukuru mbunge huyo kwa msaada huo wa madawati na kueleza kuwa uwepo wake katika jimbo hilo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo na kuifanya hatua kupiga hatua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya kasulu mji Bw. Noel Hanura ambaye ni diwani wa kata ya heru juu amemshukuru Prof. Joyce Ndalichako kwakuwa mbunge kiongozi ambaye pamoja na majukumu makubwa ya serikali aliyonayo amekua na utamaduni mzuri wa kukutana na wananchi na kutatua kero zao.
Aidha mkurugenzi wa halmashauri ya mji kasulu Bw. Dollr Kusenge amesema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya madawati ambaponhapo awali halmashauri ilikuwa na upungufu wa 22500 na pia ameendelea kumshukuru Rais SAMIA SULUHU HASSAN kwani ameboresha mazingira katika Nyanja za elimu afya na mazingira kwa kuleta watumishi wa kutosha.
Naye mkuu wa shule bogwe bw.David Kindanda kwa niaba ya wakuu wa shule na walimu wakuu wote amesema,”naishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji na kwamba madawati waliyopewa leo yatasaidia kupandisha kiwango cha taaluma na kupunguza utoro.