MENEJIMENTI YATAKIWA KUFUTA HOJA
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameitaka halmasahuri kufanya kazi kwa weledi na kusimamia miradi kwa ufanisi na kwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali hasa katttika swala zima la utoaji wa wa taarifa za fedha ili kupata ustawi Zaidi ambapo halmashauri ya mji wa kasulu imepata hati safi yenye alama 72.
Ameyasema Hayo wakati akizungumza na baraza la madiwani katika kikao maalumu cha ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali ambapo amesisitiza kuendelea kutoa mafunzo na vitendea kazi pamoja na kuhakikisha halmashauri inaimarisha ofisi ya mkaguzi wa ndani kama mfumo wa udhibiti wa ndani wa halmashauri kwa kuzingatia utaratibu ikiwa nipamoja na kuitioa fedha zote za lishe ili zikafanye jkazi ya kupunguza pengine kuondoa kabisa swala la udumavu kwenye jamii zetu.
Aidha andengenye ameendelea kusisitiza kuendelea kutumia vyema mapato ya ndani kwa kuendelea kuboreshas utoaji wa mikopo ya asilimia kumi ili kupunguza hoja ilizokuwanazo licha ya kuonyesha kutenda vyema katika ukusanyaji mapato na swala zima la utoaji mikopo ya asilimia kumi kuhakikisha inaziondoa kabisa hoja hizo na kuwasisitiza madiwani kuwahamasisha wananchi kufahamu lengo la sensamenejimenti ya na kushiriki katika kuhesabiwa ifikapoagosti 23.
Kwa upande wake wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa kasulu Bwn Dollar Rajabu Kusenge ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kutoa vibali vya kuajiri watumishi 184 ambalo litaweza kuleta ufanisi wa kazi na kuweza kupunguza hoja hizo pia kuishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa wa kigoma ambao wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu Zaidi aambalo limeweza kipatia halmashauri ya hati safi na kuhakikisha mwaka wa fedha unmaisha kwa hoja kufutwa kabisa nah ii iklitokea kutokuwa na watumishi wa kutosha wenye uwezo wa kuweza kuzijibu hoja kiufasaha na kusisitiza kuwa halmashauri itatenga fedha kwa ajili ya mafunzo ya wahasibu ili kuweza kuwaongezea ufanisi katika utendaji kwzi
Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kasulu bw,Noel Hanura amesema kuwa atahakikisha menejimenti kwa kushirikiana na baraza la madiwani wanafanya kazi kama timu kwa umoja ili halmashauri iweze kufanikiwa Zaidi kuingia katika kkundi la halmashauri zinazofanya Zaidi na kumwiomba mkuu wa mkoa wa kigoma kusaidia halmashauri iwe na barabara zenye viwango vya rami