VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI WASHIRIKI KIKAO CHA TATHIMINI YA ZOEZI LA CHANJO YA POLIO KWA AWAMU YA KWANZA
Kutokana na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa KIgoma kushindwa kutekeleza zoezi la chanjo ya polio kwa awamu ya kwanza kutokana na Imani za kidini ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa kasulu imekutana na viongozi wa madhehebu ya dini ili kuzungumza namna watakavyoshiriki zoezi kwa awamu ya pili.
Aidha mratibu wa Elimu ya Afya Bw.Marcus amesema lengo kubwa la kukutana na viongozi hao wa dini ni kupeanan mrejesho wa wa zoezi la chanjo kwa awamu ya kwanza na kuendeleza ushirikiano hususani kwenye kuhamasisha ushiriki wa jamii(waumini wao)tunapoelekea kwenye kampeni ya chanjo ya polio kwa awamu ya pili na kuendelea kuboresha afya ya wana kasulu.
Kwa upande wao viongozi hao wa madhehebu ya dini walisema,”tuko tayari kushirikiana na Idara ya afya kuhusiana na maswala yananyohusu afya na kuboresha afya kwa jamii(waumini)na tutaenda kuwa mabalozi kwa kuwahamasisha kushiriki kikamilifukwenye zoezi ya chanjo ya polio kwa awamu ya pili amabyo imatarajia kuanza tarehe 2 mpaka 5,novemba mwaka huu.