Kamati ya siasa ya Wilaya imepongeza usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Kasulu.
Pongezi hizo zimetolewa leo wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa.
Miradi hiyo iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Kimobwa iliyojengwa kupitia mradi wa SEQUIP,umaliziaji wa bwalo Shule ya sekondari Bogwe,ujenzi wa mashedi soko la mnadani kata ya Kigondo,ujenzi wa shule mpya ya sekondari mtaa wa Mkombozi,ukamilishaji wa mabweni na bwalo kupitia program ya EP4R awamu ya pili katika shule ya Sekondari Nyumbigwa Mpya na ujenzi wa Ofisi Pamoja na kituo cha Polisi katika kata ya Kumsenga kupitia mapato ya ndani na ukarabati unaoendelea katika Hospitali ya Mji Kasulu.
Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndugu Abdallah Mbelwa amepongeza mkurugenzi kwa usimamizi Madhubuti wa miradi hiyo unaofanya hata wao wao wenye ilani kuridhika.
Ndugu Mbelwa amesema Kamati imeridhishwa na kazi zinavyofanyika na thamani ya pesa iliyotumika.