Kamati ya Uchumi Elimu na Afya imetembelea na kukagua mradi wa ukarabati wa hospitali ya (W) Kasulu (Mlimani) wenye thamani ya Shilingi Millioni mia tisa (900) ambao uko mbioni kumalizika.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi Mhe. Josephine Gezabuke mbuge wa viti maalum mkoa wa kigoma ambae ni mjumbe wa kamati hiyo ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa ukarabati wa hospitali hiyo
Aidha amepongeza uongozi wa hospitali kwa usimamizi mzuri kwani hakuna malalamiko yanayoyolewa na wananchi kama ilivyokua hapo awali.
“Siku hizi huduma zinazotolewa katika vituo vya afya na hospitali ni nzuri hata ule ulalamikaji wa kuuziwa dawa haupo tena hii inaonesha namna gani uongozi unafanya kazi
Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuleta miradi mingi katika wilaya ya Kasulu kwani hapo nyuma mkoa wa Kigoma ulionekana kuwa nyuma kimaendeleo.
Lakini katika hatua nyingine ameeleza kuchukua changamoto ya upungufu wa madaktari na wahudumu wa Afya na kuiwasilisha katika mamlaka husika.