Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu Pamoja na uongozi wa shirika la DRS wameongoza baadhi ya wananchi wa kata ya nyumbigwa kupanda miti katika eneo la msitu wa Mkuti ikiwi ni mojawapo ya jitihada za kuhifadhi mazingira.
Akizungumza awali Kanali Mwakisu amesema ni jukumu la kila mwananchi kutunza mazingira ikiwemo kupanda miti ili kuokoa kizazi kijacho.
Aidha amekemea vikali wale wanaokata miti kwa kisingizio cha kulima badala yake ametaka wanaotaka kulima kufuata utaratibu ili waweze kupata ardhi kwa ajili ya kilimo.
“ukiweka miti hata mazingira yanakua mazuri kumekua na hulka ya watu kukata miti bila kufuata utaratibu kwa kisingizio cha kulima hakuna mtu anakataza kilimo ila fata utaratibu.”
Pia amewataka wanaochoma moto misutu kuacha mara moja kwani moto ni adui mkubwa wa miti hivyo amewataka wananchi kuwa walinzi wa miti ambayo inapandwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la DRS Jeremiah Mutagoma ameeleza kuwa zoezi hilo ni moja ya programu ambayo inaendeshwa na shirika lao ikiwa ni miti iliooteshwa ili kuhakikisha wanatunza hifadhi ya msitu huo ambao uliharibika kutokana na shughuli za kibinaadam.