Katika utekelezaji wa agizo la serikali la upandaji miti tayari Halmashauri ya Mji Kasulu imepanda miti mil 1.2 sawa na 80% ya miti mil 1.5 iliyolengwa kupandwa kwa mwaka 23/24
Hayo yamebainishwa na Afisa mazingira Wambura Muniko Mwita wakati wa mahijiano maalumu na redio Buha yaliyolenga utoaji wa elimu kwa umma na mikakati ya udhibiti hewa ya ukaa pamoja na namna bora ya kupandaji na kutunza miti.
Amesema Halmashauri imeunda vikundi vya mazingira kwa kila kata kwa lengo la kupanda miti na kuzuia ukatwaji wa miti pia kutumia nishati mbadala ya kupikia.
“Tuna programu ya kuzunguka kila kata kuhamasisha majiko mbadala wakitumia majiko sanifu itasaidia kupunguza ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya mkaa hivyo tunawaelemisha kutumia gesi,umeme, na mkaa mbadala.”
Ameongeza kuwa halmashauri imelenga kuweka Mji safi na kutunza vyanzo vya maji milima na kuweka mazingira rafiki kwa viumbe hai hivyo upandwaji wa mti hio umezingatia miti ya matunda,mbao,vivuli na dawa katika kata zote.