Kasulu, 9 Septemba 2025 –
Kongamano kubwa la kuliombea amani ya Taifa limefanyika Kasulu likiandaliwa na Mkuu wa Wilaya, Kanali Isaack Anthon Mwakisu, huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro.
Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali waliongoza maombi yaliyogusa watu na kumshukuru Mkuu wa Wilaya kwa maono ya kuwakutanisha pamoja. Walisisitiza kudumisha amani na kuwataka wagombea kufanya kampeni kwa utulivu na mshikamano.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Askofu Josephat Kilibaze Sebana, alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa hatua yake ya kuziunganisha dini zote kupitia kongamano hili, na kusifia hali ya amani iliyopo kwa sasa katika Wilaya ya Kasulu.
Akihutubia, Balozi Simon Sirro aliwataka wananchi wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kusikiliza kampeni kwa makini, kuchambua sera za wagombea, na kufanya maamuzi sahihi. Pia alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Septemba 2025, akisisitiza mshikamano, mshikikiano na maadili ya Kitanzania.
Kongamano hili limeacha ujumbe wa mshikikiano wa kitaifa, likiwakumbusha Watanzania wote umuhimu wa kulinda amani kama msingi wa maendeleo endelevu