Leo tarehe 14 Julai 2025, Halmashauri ya Mji wa Kasulu imefanya uzinduzi rasmi wa chanjo za mifugo kwa wanyama na ndege kama kuku na bata. Tukio hili muhimu limefanyika katika Kata ya Nyumbigwa na kuhudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Bi. Theresia Mtewele, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kama mgeni rasmi. Pia walikuwepo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, maafisa wa halmashauri, pamoja na watendaji wa kata na mitaa.
Katika hotuba yake, Bi. Mtewele alikumbusha kuwa tarehe 16 Juni 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua kampeni ya kitaifa ya uchanjaji wa mifugo, ikiwa ni hatua ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo, kukuza biashara ya nyama, na kuongeza kipato cha wafugaji. Alieleza kuwa zoezi hilo litafanyika nchi nzima, ambapo chanjo zitatolewa dhidi ya magonjwa kama homa ya mapafu ya ng’ombe, ugonjwa wa miguu na midomo, kideli, mafua ya ndege, mdondo na ndui kwa kuku na bata. Mifugo mingine itachanjwa kwa kuchangia nusu ya bei, huku kuku wakichanjwa bure.
Katika tukio hilo hilo, Halmashauri ya Mji wa Kasulu ilipokea rasmi mradi wa “Misitu Yetu Urithi Wetu” kutoka kwa shirika la DRST, kwa ufadhili wa GEF/UNDP. Mradi huo umekabidhiwa kwa vikundi vya wajasiriamali wa Kata ya Nyumbigwa na sasa viko chini ya usimamizi wa halmashauri.
Vikundi vilivyonufaika ni: