Mganga mkuu mkoa wa kigoma Dkt. Jesca Lebeea aweka wazi malengo ya mkoa wa Kigoma katika kutokomeza ukimwi toka asilimia 1.7 mpaka 0 wakati Akihutubia mapema Leo hii.
Amebainisha hayo kwenye utambulisho wa Mradi wa kupunguza umaskini kwa watu wanaoishi na VVU kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda pamoja na kutoa uelewa dawa za kupunguza makali ya VVU na kipimo cha jipime hususani kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wilayani Kasulu chini ya shirika la Disabilities Relief services (DRS) kupitia ufadhili wa ubalozi wa Marekani.
Amesema kuwa kuondoa maambukizi ya Ukimwi na kumfikia sifuri inawezekana ikiwa uzingatiaji wa lishe bora kwa wahanga utazingatiwa.
"kama mkoa lengo kuu ni kushusha maambukizi mpaka tufikie 0% kama tumetoka 2.9% mpaka 1.7% basi inawezekana lakini ni kuongeza hadhi ya lishe pamoja na kuwa miongoni mwa mikoa yenye udumavu ya lishe lakini kwa kuwekeza kwenye elimu tunaweza tatua changamoto hii."
Ameongeza kuwa iwapo itaonekana kuna uhitaji watapeleka ushauri wa upatikanaji wa Prep maeneo mbalimbali nje ya vituo vya Afya (madukaya madawa) ikiwa sera ya wizara ya Afya inataka hivyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa DRS Jeremia Mutagos amesema mradi umelenga kuwezesha wahusika kupata chakula pamoja na kujikimu ndio maana hasa wameelekeza katika kilimo cha mboga mboga na matunda.
"Tumelenga kwenye kilimo cha mboga mboga ili kusaidia waathirika kwanza kupata lishe bora lakini pia mboga na matunda wanaweza kuuza ili kupata nauli ya kufatia dawa Kwani wengi wamekua wakikosa nauli ya kuhudhuria katika vituo vya Afya."
Mradi huo ambao utanufaisha kata tano wilayani Kasulu tatu tokea Halmashauri ya mji ikiwa kata ya Kimobwa, Murubona na Murusi kwa kipindi cha mwaka Mmoja ukigharimu kiasi cha dola 25,000 Sawa na Millioni 60 za kitanzania.