Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Mh.Joyce Ndalichako leo amekuwa mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya kugawa majiko banifu kwa wanufaika wa TASAF iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kasulu.
Katika taarifa yake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Nurfus Aziz Ndee amesema Ofisi yake ilipokea jumla ya majiko 352 kutoka kwa Wakala wa nishati vijijini (REA) ambayo yanatakiwa kugawiwa kwa wanufaika wa Tasaf kutoka kata nane na mitaa tisa.
Mheshimiwa Ndalichako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini amewapongeza wanawake walioshiriki hafla hiyo kwa kuazimisha siku ya wanawake duniani leo na kuwaomba kuyatumia majiko banifu vizuri ambayo yanatumia mkaa kidogo na kuni kidogo.
Aidha Mheshimiwa Ndalichako amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Rais Samia Suruhu Hassan kwa kuleta majiko ya nishati safi ya kupika ili kuokoa mda na kulinda mazingira
Naye Mtaalam jinsia ya Nishati toka Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Dr Joseph Sambali amewahimiza wanufaika hao wa majiko hayo banifu kuyatumia vizuri kwani yameandaliwa ili kuokoa mazingira yetu Pamoja na afya zetu,
Naye mnufaika wa majiko hayo banifu Bi Fatuma Gitabwa kutoka Kata ya Nyansha ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayoongozwa na Dr Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia majiko hayo ambayo kwa ujumla yatawasaidia sana.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mh Noe Hanura aliyemshukuru mtaalamu wa jinsia na nishati vijijini (REA ) kwa kuwakomboa wanawake ambao kwa kutumia majiko haya banifu watatumia mkaa kidogo lakini pia na kuni kidogo.