Leo Oktoba 07 madaktari bingwa katika fani mbali mbali wamefika Halmashauri ya Mji kasulu na kuanza kutoa matibabu kwa wananchi kama ilivyotangazwa hapo awali
Akizungumza Kiongozi wa jopo hilo Dkt Innocent Kaiza bingwa wa magonjwa ya kina mama amesema lengo la wao kufika ni kutekeleza mpango wa serikali katika kuboresha huduma za afya kwa watanzania wote.
“Sisi tumeagizwa na serikali kupita katika Halmashauri zote nchini kwa lengo la kutoa huduma za matibabu ya kibingwa.“
Ameongeza kuwa awamu hii wanategemea kuhudumia wananchi wengi zaidi kwani awali katika awamu ya kwanza programu hio imeonesha mafanikio hivyo serikali imeona umuhimu wa kuendelea kuwafikia wananchi wenye changamoto.
Pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupata matibabu ya kibingwa toka kwenye timu hiyo ya madaktari.
Ikumbukwe kuwa madaktari hao watakua katika Halmashauri ya mji kwa Juma moja kuanzia oktoba 7 mpaka 12 ikiwa imejumuisha madaktari bingwa wa kina mama, watoto, kifupi, afya ya kinywa na meno, upasuaji na magonjwa ya ndani.
@ortamisemi @kigomars @ofisiya_mkuu_wa_wilaya_kasulu @vumysimbeye @kasuludistrictcouncil @kasulu_town_council