WATENDAJI WA KATA NA MITAA WAPATIWA MAFUNZO YA O&OD ILIYOBORESHWA
Watendaji wa kata 15 za halmashauri ya mji wa kasulu wamepatiwa mafunzo ya fursa na vikwazo iliyoboreshwa katika kupanga mipango ya bajeti ambayo lengo lake kuwajengea uwezo na uelewa watendaji hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa jamii na mamlaka ya serikali na mitaa.
”mfumo wa O&OD ambayo haikuboreshwa inazungumzia kuongezeka kwa utegemezi,ushiriki hafifu ikimaanisha wanajamii wengi kutoshiriki pia ukosefu wa umiliki pia kuna faida ya uboreshwaji wa mfumo wa fursa na vikwazo iliyoboreshwa ambazo ni pamoja na kuchochea maendeleo endelevu,kuhakikisha jamii imejengewa uwezo wa kutekeleza mipango ya maendeleo kupitia jitihada zao, kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya jamii na mamalaka za serikali za mitaa katika utoaji huduma na kuleta maendeleo katika ngazi za msingi,”alisema bw.Nurfus Ndee ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw.Gilbert Rutaihwa ambaye ni afisa mipango wa halmashauri ya mji alisema matarajio yao baada ya kutoa mafunzo hayo ni kutengeneza mipango na bajeti kwa kutumia mfumo wa fursana vikwazo(O&OD)iliyoboreshwa kwa kuwashirikisha wananchi katika mipango na bajeti kwa kutumia mfumo huo.
Aidha baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema,”mafunzo hayo ni mazuri na tumeyapokea tutashirikiana na jamii kwaajili ya kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu wa fursa na vikwazo ulioboreshwa”.