Halmashauri ya Mji Kasulu inatekeleza mpango wa serikali na shirika la afya Duniani(WHO) wa kuhakikisha kuwa tunafikia asilimia 80 ya matumizi ya byandarua kwenye jamii,hivyo kupitia mfuko wa Global Fund na bohari yad awa ya Taifa (MSD)imepanga kuendesha zoezi hilo kwenye kata zote 15 zilizopo Halmashauri ya Mji.
Zoezi la kampeni ya ugawaji wa vyandarua kwenye kaya lilianza na uraghabishaji kwa viongozi ngazi zote, mafunzo kwa watendaji pamoja na wandikishaji ambapo mpaka sasa watendaji wa kata 15, watendaji wa mitaa 45 na waandikishaji 90 wameshapatiwa mafunzo na zoezi la uandikishaji wa kaya zote limeshaanza ili kubaini idadi halisi ya vyandarua katika kila kaya.
Mpaka sasa kaya zipatazo 18,536 kati ya 50,305 zimekwisha kusajiliwa katika mfumo maalum na zoezi la uandikishaji linaendelea.