Wananchi wa Kata ya Kumnyika, Halmashauri ya Mji Kasulu, sasa wamepata nafuu kubwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shedi mbili za kisasa katika soko lao, mradi uliogharimu shilingi milioni 70 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mradi huu ulioanza Februari 2025 na sasa kukamilika kwa asilimia 100, umeondoa changamoto ya jua na mvua iliyokuwa ikiwakabili wafanyabiashara waliokuwa wakifanya shughuli zao chini bila kinga.
Wananchi kwa furaha kubwa wamemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia J. Simbeye, kwa jitihada za kuhakikisha mapato ya ndani yanatumika kuboresha maisha yao.
Mbali na soko la Mnarani, mapato ya ndani yameendelea kugharamia miradi mbalimbali ikiwemo: