Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac
Mwakisu katika kikao cha jukwaa la mwaka kwa mashirika yasiyo ya
kiserikali NGOs ndani ya ukumbi wa mkutano wa mkuu wa wilaya.
Wadau wa maendeleo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameshauriwa
kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha jamii utunzaji wa
mazingira ili kuepuka kuchoma misitu moto na kuona umuhimu wa
utunzaji wa mazingira.
Amesema lengo la kuwashirikisha wadau hao wa maendeleo ni kufuatia
baadhi ya wananchi kuchoma misitu moto kutokana na fikra hasi hali
inayopelekea uharibifu wa mazingira ndani ya wilayani hiyo.
Aidha Kanali Mwakisu amesema serikali tayari imeandaa mpango wa
kuwakamata wale wanaochoma misitu moto.
Nao baadhi ya wadau wa maendeleo wilayani Kasulu wamesema
wanatambua umuhimu wa kutunza mazingira huku wakionyesha utayari
wao wa kushirikiana na serikali katika suala hilo.