Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini profesa Joyce Lazaro Ndalichako amewataka wanawako kuendelea kujishughulisha katika Nyanja za uchumi kupitia ujasiriamamli na kutumia vyereheni hivyo katika mahitaji yaliyokusudiwa ili kujikwamua katika hali duni.
Aliyasema hayo wakati wa ziara yake jimboni humo wakati wa zoezi la ugawaji wa vyerehani 100 kwa vikundi 25 vya wajasiriamali wanawake kwa wanaume mjini kasulu vyenye thamani ya shilingi Zaidi ya milioni 30 kutoka nchini China kupitia balozi wake nchini Tanzania ikiwa ni harakati za kumwinuab mwanamke kiuchumi.
Kwa upande wao baadhi ya wanawake wanufaika wa vyerehani hivyo wamesema kupatikana kwa vyereheni hivyo kutoka kwa mbunge wao ni chachu ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia kuinua pato ya familia,halmashauri na taifa kwa ujumla.