Mbunge ya Jimbo la Kasulu Mjini Mkoani Kigoma Mhe. Prof. JOYCE LAZARO NDALICHAKO amehitimisha ziara yake ya siku tano za kikazi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu.Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mbunge aligawa Mashine ya kurudufia karatasi na sare za wanafunzi katika Shule ya Msingi Marumba, vifaa vya wajawazito wakati wa kujifungua, vyandarua kwa ajili ya wajawazito na watoto sambamba na kuweka mawe ya ufunguzi na kufungua rasmi baadhi ya Shule za Msingi na vituo vya afya n.k.
Ziara hiyo ilianza tarehe 25.4.2025, Katika ziara hiyo ya kikazi ,amefanya mambo mbalimbali ikiwemo kuweka mawe ya msingi shule ya msingi Mnyika na Sekondari ya Msambara kata ya Msambara, ameshiriki zoezi la utoaji mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi, uzinduzi wa shule ya msingi Ndalichako iliyoko kata ya Murusi na kuweka jiwe la msingi kituo cha afya Nyansha na ugawaji wa vyandarua na seti za kujifungulia katika kituo hicho cha afya Nyansha.
Aidha Mheshimiwa Ndalichako katika Kata ya Murubona ametembelea kituo cha afya cha Kiganamo na Hospitali ya Wilaya ambapo ameshiriki katika zoezi la kugawa taulo za kike.
Kata ya Heru Juu amefika Zahanati ya Heru Juu na kugawa seti za kujifungulia, ameiembelea Kata ya Muhunga kituo cha afya Muhunga na kugawa vyandarua katika kituo hicho ,ametembelea Sekondary za Mhunga na Marumba.
Mheshimiwa Ndalichako amekagua ujenzi wa stendi ya Kumnyika, ujenzi wa soko la sofya, uwekaji wa kifusi eneo la mnadani na ujenzi shedi ya abiria pamoja na daraja la Nyantare.
Kipekee alimshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suruhu Hassan kwa juhudi zake kubwa za kuleta fedha za miradi ya maendeleo kwa kipindi chote cha miaka minne. Katika ziara hiyo ya kikazi aliambana pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mwalimu VUMILIA SIMBEYE ambaye amesema anashuru sana kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Ofisi ya Mheshimiwa Mbunge na Halmashauri ya Mji wa Kasulu na kumhakikishia kuwa; ushirikiano huu utaendelea wakati wote.
Katika ziara hiyo wananchi wamefarijika sana na kumshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa ujio wake ambapo wamesema wanaimani kubwa na Mbunge huyo. Kazi na utu,
Tunasonga mbele.