MWENGE WA UHURU 2023 WATEMBELEA, KUZINDUA NA KUFUNGUA MIRADI MIINE YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MJI KASULU
Mwenge wa uhuru 2023 umepitia miradi 4 halmashauri ya mji ambapo kati ya hiyo miwili itazinduliwa ,mmoja utatembelewa na mmoja utafunguliwa na miradi yote hiyo imegharimu kiasi cha shilingi 714,952,439.80 mpaka kukamilika ambapo wananchi walichangia kiasi cha shilingi 20,200,000.00 ,serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi 40,000,000.00 ,halmashauri imechangia kiasi cha shilingi 184,903,870.80 na wahisani wamechangia kiasi cha shilingi 469,848,569.00 na miradi hiyo ni kikundi cha uselemara kikosi kazi IPOSA,nyumba ya watumishi kituo cha afya Nyansha,mradi wa Maji Hwazi na vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi mwibuye.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Prof.JOYCE LAZARO NDALICHAKO kuwa,”serikali ya awamu ya sita imeendelea kuboresha mazingira katika miundo mbinu ya afya,maji,elimu na barabara ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua katika kudhibiti vitendo vya rushwa ikiwemo kuanzisha tume ya haki jinai hivyo niwaombe wananchi wangu wa mji wa kasulu tuendelee kutoa ushirikiano haswa linapokuja swala la maendeleo na nawasihi vijana muwe wazalendo katika kuitumikia nchi katika Nyanja mbalimbali”.
Aidha kiongozi wa wakimbizwa mwenge kwa mwaka 2023 bw.Abdalah Shaibu Kaim alisema rushwa ni adui wa haki na imekuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo kwa baadhi ya maeneo na amewashukuru wananchi kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kwene maeneo yao na kwamba “mwenge wa uhuru umeridhika na miradi hii na kuanzia sasa ianze kutumika”.
Naye mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu amewashukuru wananchi wa wilaya ya kasulu kwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge huu na kuwasisitiza wataalamu kwenye halmashauri kutoa ushirikiano kwa viongozi mbali mbali wanapofika kufanya ukaguzi katika miradi iliyopo kwenye maeneo yao.