Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu bw. Dollar Rajab Kusenge ametoa maagizo kwa Afisa Elimu Sekondari pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Muka kuhahikisha wanaongeza nguvu kazi ya mafundi pamoja na muda wa kufanya ili kuweza kukamilisha kwa wakati miradi ya maendeleo inayotekelezwa shuleni hapo
Aliyasema hayo wakati wa ziara fupi ya ukaguzi wa maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali iliyopo shule ya sekondari MUKA na kusisitiza,”inatakiwa muweke daftari la kusaini kwenye haya maeneo mnayofanyia kazi na pia mafundi na wasimamizi wote muweke kambi maeneo yenu ya kazi kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi kwa wakati”.
Aidha kusenge ameendelea kusisitiza kufungwa taa kwenye miradi ambayo bado iko nyuma kwenye utekelezaji ili kazi zifanyike usiki na mchana ili kuepuka kuchelewesha kazi kuisha kwa wakati na kuwa na miradi isiyo bora na kuchelewesha upatikanaji wa huduma ya elimu kwa walengwa .
Katika ziara hiyo ametembelea miradi miwili ambayo vyumba saba vya madarasa vitakavyogharimu kiasi cha shilingi 182,000,000/= ,matundu kumi na saba ya vyoo yatakayogharimu 37,400,000/= na mabweni mawili yatakayogharimu kiasi cha shilingi 139,000,000/= mpaka miradi hiyo inakamilika na fedha zimetoka serikali kuu.