Katika hotuba yake leo Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mheshimiwa Col. Isaac Anton Mwakisu ametaja mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika maazimisho ya siku ya Muungano yaliyofanyika kwenye viwanja vya Umoja ni imani Halmashauri ya Mji wa Kasulu .
Amesema kuwa mafanikio yapo mengi, katika kipindi cha miaka sitini na moja ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa tarehe 26.4.1964 (siku ya Jumapili) umeleta mafanikio makubwa yanayoonekana katika nyanja mbalimbali ya maisha ya wananchi wa pande zote mbili.
Mwakisu ambaye alikuwa mgeni rasmi ametaja kuwa muungano huu ni wa kipekee uliojengwa kwenye msingi wa maelewano, mshikamano na dhamira ya pamoja ya kujenga taifa lenye haki usawa na maendeleo kwa wananchi wote.
Kupitia Muungano huu tumejenga miundombinu imara ya umeme, barabara, nishati na usafirishaji,biashara na uwekezaji, elimu afya , kilimo,Maji na mambo lukuki yanayoonekana kwa wananchi,
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuutunza ,kuuenzi muungano na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili kuimarisha demokrasia ambayo ni mafanikio ya muungano.
Kauli mbiu ya maazmisho ilikuwa MUUNGANO WETU NI DHAMANA HESHIMA NA TUNU YA TAIFA SHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025.