Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col. Isack Mwakisu akitoa mikopo ya Vijana, Wanawake na Walemavu toka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Kasulu. mkopo wenye jumla ya Sh. 134M . Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Leo 2.2.2022 . Mkopo huo umetolewa kwa vikundi 4 ,ambapo 2ni vikundi vya vijana na 2 ni vikundi vya wanawake . Vikundi hivyo ni ni kikundi cha vijana cha Studio vijan kilichopata mkopo wa Sh. 12M, Kikundi cha vijana cha Kikosi Kazi IPOSA Kalema kilichopata mkopo wa mashine za uselemala zenye thamani ya Sh.110M,Kikundi cha wanawake kwa mradi wa ufugaji nguruwe mkopo wa Sh. 7M na kikundi cha wanawake cha Msaneza kwa mradi wa ushonaji mkopo wa Sh. 5M