Leo tarehe 04/03/2025 limeanza zoezi la utoaji majiko ya gesi katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma.
Zoezi hIli limefanyika kwa mwitikio mkubwa sana wa wananchi ambapo kila mwananchi alitakiwa kuwa na kitambulisho cha NIDA pamoja na elfu ishirini tu, Gharama zingine ni ruzuku ya Serikali.
Katika zoezi hili liloanza leo jumla ya majiko ya gesi elfu moja mia sita ishiri na nane (1,628) yanategemewa kuwafikia wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Mpaka sasa Zaidi ya majiko ya gesi mia mbili yamekwishagawiwa kwa wananchi.
Akizungumza na mwandishi wetu Bi Sarah Esau ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta Nishati hii safi ambayo sasa wanaenda kuitumia kupika chakula kilichobora zaidi na kupika kwa kujiamini.
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Ndugu Wambura Muniko amesema zoezi hili linaendelea vizuri na kwamba kesho wataendelea na Kata ya Kumnyika. KAZI IENDELEE.