MKUU WA MKOA WA KIGOMA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BOOST
Watendaji kazi wa serikali mkoani kigoma wametakiwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa umakini na uadilifu ili kutokuwa kikwazo kwa serikali katika kuwafikishia huduma mbalimbali wananchi.
Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa kigoma mheshimiwa thobiasi andengenye wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya BOST na SEQUIP kusisitiza wataalamu kufanya tathinini na kufuatilia utekelezaji wa miradi wakati wote.
Aidha andengenye ameendelea kusema, watendaji wa serikali mnapaswa kuepuka kuzipa nafasi changamoto zinazojitokeza wakati wa kukamilisha miradi na kuzifanya kuwa sababu ya kushindwa kufikia malengo yakiyowekwa ,muwe wawazi na kutumia mbinu shirikishi katika kutafuta suuhisho ya cangamoto na hakuna sababu ya kushindwa kukamilisha miradi wakati serikali imeshalet fedha za kutosha kaika maeneo miradi ya maendeleo inakotekelezwa.
Kupitia ziara hiyo mkuu wa mkoa ametembelea na kukagua ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali kwaajili ya uboreshaji wmazinira ya ufundishaji na ujifunzaji chini na program za BOOST na SEQUIP katika shule za sekondari Nyumbigwa mpya,muka,msambara npamoja shule za msingi kasulu,nyansha na kibagwe na kukamilika kwa miradi hiyo kutapunguza mlundikano wa wanafunzi madarasani ,vyooni pamoja na kpunguza umbali wa kuyafika maeneo ya kutolea huduma za kitaaluma.