Leo Julai 8, 2025, Mkuu mpya wa Mkoa wa Kigoma, Kamanda mstaafu Saimon Nyakoro Siro, amewasili Kasulu kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushika nafasi hiyo baada ya kustaafu kutoka Jeshi la Polisi na pia kulitumikia taifa kama Balozi.
Akipokelewa kwa heshima na furaha kubwa, Kamanda Siro alipokelewa na viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu na Kasulu Vijijini, wakurugenzi, wabunge, viongozi wa dini, taasisi za serikali, na wawakilishi wa vyama vya siasa.
Wananchi wa Kasulu wameonesha matumaini makubwa kwa uongozi wake, wakimkaribisha kwa moyo mkunjufu huku wakieleza imani yao katika