TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE KWA ROBO YA JULAI-SEPTEMBA YAFANYIKA IKIWASHIRIKISHA WATENDAJI WA KATA 15 ZA HALMASHAURI YA MJI
Maafisa lishe wa halmashauri watakiwa kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusiana na maswala ya lishe kwani baadhi ya wananchi hawafahamu namna ya kupangilia vyakula vya lishe ingawa wana vyakula vingi.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Bi Telesia Mtewele ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya kasulu katika kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe julai mpaka septemba alisema,”andaeni ratiba za kuwafuata watu huko waliko kuliko kusubiri mpaka mpate hela ndo muwaite na ninyi watendaji mkasimamie kwenye shule mbazo hawatoi chakula ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha jamii katika kushiriki maadhimisho ya lishe kwenye mitaa yao hivyo mnatakiwa kuhakikisha fedha zinazotolewa zinafanya kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha kunakuwa na mpango jumuishi wa lishe katika maeneo yenu ya kiutawala mpaka kwenye jamii kwani bado kunaonekana watoto wengi wamedumaa”.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Bi Paschalina Mabena alisema,”ninawaomba ninyi watendaji mshirikiane na maafisa wa lishe kuendelea kutoa elimu kwaakina mama kuhusu kuacha kujifungulia nyumbani badala yake wakajifungulie kwenye vituo vya afya pamoja na maswala ya lishe hii itasaidia kuwa na jamii yenye afya bora”.
Naye afisa lishe wa halmashauri ya mji wa kasulu Bw.Mwita Range alisema ,”kwasasa mwitikio wa jamii kushiriki maswala ya lishe umekuwa mkubwa hali inayopelekea kupunguza utapiamlo kwa watoto lakini pia kuchangia jiko darasa kwenye kata ili kuweza kufanikisha zoezi la lishe kwenye jamii na kuwaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi na pia kufuata ushauri wanaopewa na maafisa lishe wanapopita kwenye maeneo yao”.
Kwasasa hali ya lishe kwa halmashauri ya mji inaendelea vizuri kwani wimbi la watoto wenye utapiamlo limepungua kwa asilimia 90% ukilinganisha na hapo awali ambapo jamii nyingi zilikuwa hazina uelelwa na elimu kuhusu maswala ya lishe na namna ya kupangilia mlo kamili licha ya kulima na kuwa na vyakula vingi.