UBORESHAJI UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI JUMUISHI KUSAIDIA KUINUA TAALUMA MKOANI KIGOMA
Walimu mkoani kigoma wametakiwa kutumia mbinu mbalimbali ziliboreshwa kufundishia na kujifunzia ili kuweza kuinua taaluma na kuwajengea uwezo watoto wenye mahitaji maalumu kushiriki kwa ufasaha katika kujifunza.
Hayo yalisemwa na mkufunzi wa mafunzo ya kitaifa kuhusu uboreshaji ufundishaji na ujifunzaji jumuishi bw.Amos kazimili machemba ambaye ni Mkufunzi wa chuo cha ualimu kasulu na kusema”lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha walimu namna ya kuwabaini watoto wenye mahitaji maalumu pia kupata mbinu za kufundishia madarasa jumuishi na kuhakikisha kunakuwa na miundo mbinu rafiki inayoweza kufikika kwa urahisi na uwezeshaji katika jumuiya ya kujifunzia”.
Aidha Machema ameendelea kusema,”matarajio yetu baada ya mafunzo haya mwalimu aliyepata mafunzo haya ataenda kuwafundisha walimu wengine kwenye shule kuhusiana na namna ya kuwatambua na kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalumu na tunatarajia wanafunzi pia watajifunza katika mazingira rafiki na yanayovutia kujifunza na kusonga mbele katika Nyanja hii ya elimu.
Kwa upande wao baadhi ya walimu kutoka shulembalimbali mkoani humu walioshiriki mafunzo hayo walisema,”kuwa vikwazo ambavyo wamekuwa wakikutana navyo katika ufundishaji wa madarasa jumuishi ni pamoja na wazazi wengi kuwaficha watoto wenye mahitaji maalumu,uelewa mdogo wa jamii kuhusu elimu,miundo mbinu isiyorafiki kama vyoo,madarasa,maji na umeme,upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia na Imani potofu pia walimu hao wameeleza kuwa watatumia mbinu mbalimbali ili kusaidia kutoa elimu jumuishi kama vikao mbalimbali na wazazi,uwepo wa miundo mbinu rafiki ya madarasa na vyoo vya kisasa,walimu kupata mafunzo ya mara kwa mara kuhusu elimu jumuishi,kupunguza adhabu kali na kufaragua zana za kufundishia kulingana na mazingira na kuahidi kuhakikisha wanapandisha taaluma mkoani kigoma”.
Jumla ya washiriki 95 wameshiriki mafunzo haya ya siku nne ambayo yanatarajia kumalizika agosti 4 ambapo waratibu kata,walimu wakuu,walimu,maafisa taaluma,afisa elimu wa mji na mwakilishi wa afisa elimu mkoa ambao kwa upande wa viongozi walipata mafunzo kwa