Leo umefanyika uzinduzi wa utafiti kuhusu usalama na ujumuishi utakaofanyika katika mikoa minne umezinduliwa Halmashauri ya Mji Kasulu.
katika uzinduzi huo mgeni rasmi Kamina wa Elimu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dr Lyabwene Mutahabwa amesema utafiti huo wa utahusisha Mikoa minne ambayo ni MKoa wa Mara -Wilaya ya BUtiama’; Mkoa wa Rukwa Manispaa ya Sumbawanga’,Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kibaha na Mkoa wa Kigoma Halmashauri ya Mji wa Kasulu.
Sababu za uchaguzi wa Mikoa hii ni tofauti zao za kiuchumi,Kijamii na Kiutamaduni, uwepo wa changamoto katika elimu jumuishi na usalama wa wanafunzi shuleni na utayari wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kushiriki katika utafiti huu.
Lengo kuu la utafiti ni kuja na suluhisho la changamoto za kukosekana kwa mfanano kwenye utekelezaji wa taratibu za usalama mashuleni,Kiwango kisichoridhisha cha utekelezaji wa elimu jumuishi shule zikiwa na mapungufu katika kutoa msaada kwa watoto wenye ulemavu na wanafunzi wengine wenye mapungufu na ushiriki mdogo wa jamii katika kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu.
Dr. Mutahabwa amesema watoto wana thamani kubwa kuliko rasilimali zingine na kwamba wanahitaji usalama kwa ajili ya ustawi wa maendeleo yao.Aidha kila kiongozi katika utendaji wake anatakiwa kuwalinda watoto ili waweze kutimiza ndoto zao.
Uzinduzi huo Pamoja na viongozi wengine umehudhuriwa na Afisa Elimu Mkoa Bi Paulina Ndigeze aliyemuakilisha Katibu Tawala wa Mkoa ambapo amehaidi kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha wakati wa utafiti huu kuhusu usalama na ujumuishi wa wanafunzi shuleni.