• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Kasulu Town Council
Kasulu Town Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Kasulu Town Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Department
      • ELIMU SEKONDARI
      • ELIMU AWALI NA MSINGI
        • MAENDELEO YA JAMII
      • MAENDELEO YA JAMII
      • MIUNDOMBINU MAENDELEO YA MJINI NA VIJIJINI
      • HUDUMA ZA AFYA USTAWI WA JAMII NA LISHE
      • VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI
      • KILIMO MIFUGO NA UVUVI
      • MIPANGO NA URATIBU
      • UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU
    • Units
      • USIMAMIZI WA TAKA NGUMU NA USAFI WA MAZINGIRA
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • FEDHA NA UHASIBU
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA UNUNUZI
      • TEHAMA
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • NMALIASILI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
      • MALIASILI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
  • Investment opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Agriculture
  • Councillors
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Ratiba
      • Ratiba
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipango Miji Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Uchumi Elimu Afya na Maji
  • Projects
    • Proposed Projects
    • On-going-Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Brochures
    • By Law
    • Strategic Plan
    • Reports
  • Media Centre
    • Video
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

VUMILIA J. SIMBEYE AHIMIZA USHIRIKIANO NA UWAJIBIKAJI KUFIKIA UFAULU WA ASILIMIA 95

Posted on: February 6th, 2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia J. Simbeye, amewataka Watendaji wa sekta ya Elimu kuimarisha ushirikiano, uwajibikaji na nidhamu kazini ili kufikia lengo la ufaulu wa asilimia 95. Amesema mafanikio katika elimu hayawezi kupatikana bila kufanya kazi kama Timu moja. Simbeye ameyasema hayo leo wakati akifungua Kikao cha Tathmini ya maMkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Mwl. Vumilia J. Simbeye, amewataka watendaji wa sekta ya elimu kuimarisha ushirikiano, uwajibikaji na nidhamu kazini ili kufikia lengo la ufaulu wa asilimia 95. Amesema mafanikio katika elimu hayawezi kupatikana bila kufanya kazi kwa pamoja. Simbeye ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao cha tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne na Upimaji wa Kidato cha Pili kwa mwaka 2025 kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji.


Katika kikao hicho, Simbeye aliwapongeza Maafisa Elimu kwa kuandaa kikao cha tathmini, akieleza kuwa ni jukwaa muhimu la kujadili mafanikio na changamoto za elimu. Aidha aliipongeza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Wadhibiti Ubora wa Shule, Wakuu wa Shule pamoja na Maafisa Elimu Kata kwa mchango wao katika matokeo yaliyopatikana.


Pia, alizipongeza shule zilizofanikiwa kufuta daraja sifuri, akisema hatua hiyo imedhihirisha kuwa azma ya Halmashauri ya kuondoa sifuri inawezekana endapo kutakuwa na mshikamano na uwajibikaji endelevu.


Aidha, Simbeye alisisitiza umuhimu wa heshima, upendo na mawasiliano kazini, huku akiwataka watendaji kuzithamini nafasi walizopewa; sambama na kufanya kazi kwa bidii. Ameutangaza mwaka huu 2026 kuwa ni mwaka wa ushirikiano na akawahimiza wakuu wa shule kuwasikiliza walimu na kushughulikia changamoto zao kwa wakati.


Amehimiza nidhamu, kuwahi kazini na kuonya dhidi ya uzembe, akisema atafanya ziara za kushtukiza ili kubaini utekelezaji wa majukumu. Aidha ameonya tabia ya baadhi ya watendaji kujihusisha na shughuli binafsi wakati wa saa za kazi.


Katika masuala ya kitaaluma, aligusia changamoto ya utoro wa wanafunzi na kuwakumbusha walimu wa madarasa kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi kwa karibu. Pia aliwaagiza wakuu wa shule za Sekondari kuandaa mikakati ya kuinua ufaulu na kudhibiti utoro.


Awali, Kaimu Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri, Bw. Jeremia Ntiboneka, amesema shule nyingi zimefanya vizuri na kutimiza lengo la kufuta daraja sifuri. Amesema lengo la mwaka huu ni kufikia ufaulu wa asilimia 95. Kwa mujibu wa takwimu, ufaulu wa Kidato cha Nne umefikia asilimia 92.75 huku Upimaji wa Kidato cha Pili ukiwa asilimia 76.


Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao hicho, Wakuu wa Shule wakiwakilishwa na Mwl. Juma Fwaya Demwa, Mkuu wa Shule ya Sekondari Murufiti, amepongeza kuandaliwa kwa kikao hicho akisema kimewasaidia wakuu wa shule kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha ufaulu.


Naye Bw. Jeremia Ntiboneka ameahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha matokeo ya elimu yanaendelea kuimarika.

Announcements

  • NAFASI ZA KAZI March 19, 2025
  • TANGAZO LA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA April 30, 2025
  • TANGAZO LA KAZI July 01, 2025
  • View All

Latest News

  • VUMILIA J. SIMBEYE AHIMIZA USHIRIKIANO NA UWAJIBIKAJI KUFIKIA UFAULU WA ASILIMIA 95

    February 06, 2026
  • KASULU YAWEKA MSINGI IMARA WA MAENDELEO ENDELEVU

    February 04, 2026
  • KARIBU KASULU MJI

    February 03, 2026
  • VIONGOZI WA DINI WAASWA KUTUMIA MAJUKWAA NA USHAWISHI WAO KUTOKOMEZA UKATILI KATIKA JAMII

    January 21, 2026
  • View All

Video

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
More Videos

Quick Links

  • News

Related Links

  • TAMISEMI
  • Ega
  • Utumishi
  • Kigoma Region

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Test

Copyright ©2017 Kasulu Town Council. All rights reserved.