Leo Oktoba 5 Mwongozo na Kanuni zauchaguzi wa viongozi wa ngazi za Vijiji, Vitongoji naMitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 umekabidhiwa kwa viongozi wa vyama vya siasa Halmashauri ya Mji Kasulu.
Viongozi wa vyama vya siasa walioshiriki ni pamoja na Mwenyekiti na Katibu wa chama Mapinduzi CHADEMA ACT Wazalendo na CUF.
Akikabidhi mwongozo na Kanuni hizo msimamizi wauchaguzi Ndugu Vumilia J. Sembeye amesema mwongozo huu wa uchaguzi umeandaliwa kwa lengo kufafanua kwa lugha rahisi maudhui ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi za msingi.
Ametaja kuwa kwa mujibu wa mwongozo na Kanuni vilivyokabidhiwa kwa ngazi za msingi za Serikali za Mitaa zina maana ya Mitaa katika Mamlaka za Miji,, Vijiji na Vitongoji katika Mamlaka za Miji zenye Vijijina Vitongoji.
Amesema kuwa mwongozo huu utawasaidia Wasimamizi Wasaidizi, Wasimamizi wavituo vya uchaguzi na wadau wengine wa Uchaguzi waweze kufahamu majukumu yao katika kusimamia mchakato mzima wa Uchaguzi, Mwongozi huu utawezesha wadau wa Uchaguzi, Pamoja na mambo mengine kufahamu haki na wajibu wa vyama vyasiasa na wapiga kura.
Pia amesisitizaViongozi hao kuendelea kuhamamisha wananchi kujitokeza kujiandikisha ili waweze kupiga Kura.
Jumla ya vituo mia mbili ishirini na tano (225)vitatumika kwenye uchaguzi huu katika Halmashauriya Mji Kasulu huku Vituo miambili ishirini na nne( 224 )viko kwenye majengo ya umma na kituo kimoja kitakua cha wazi.