Wajasiriamali wadogowadogo wa halmashauri yqa mji wa kasulu wamepewa semina ya siku moja inayohusu matumizi na faida za kitambulisho cha mjasiriamali ambavyo vinatolewa na serikali ya awamu ya sita ambayo lengo la kutolewa vitambulisho hivi ni kuwapunguzia baadhi ya tozo wafanyabiashara hao.
Hayo yamesemwa na mratibu wa zoezi la usajili na utambuzi wa wajasiriamali wadogo Bi,Rebecca Mpango leo hii wakati wa utoaji mafunzo hayo na kusema,”kitambulisho hiki kinafaida kubwa kwasababu kinamtambulisha na kinamsaidia kufanya biashara bila usumbufu na pia kimelenga makundi matatu ambao ni mamalishe na babalishe wanaotoa huduma za chakula ,waendesha pikipiki na bajaji pamoja na machinga hivyo nawasihi wajasiriamamli wajitokeze kwa wingi ili kuweza kupata vitambulisho hivi na zoezi hili limeshaanza na anaishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.SAMIA SULUHU HASSAN ambaye ameweza kuwakumbuka wajasiriamali hawa".
Aidha Afisa Maendeleo wa Kata ya Kimobwa Bi.Catherine Mchiro amesema jukumu lao kama walezi kwenye kata hizo kwanza ni kutoa elimu na kuwahamasisha wajasiriamali wapate vitambulisho na kuwasajiri wafanyabiashara hao huu akisema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni baadhi ya wajasirliamali kutaja gharama za upatikanaji wa vitambulisho hivyo iko juu hii ni kutokana na kuendelea kulipa baadhi ya tozo kuendelea kuwepo ambazo kwa msimu uliopita walikuwa wakilipia kitambulisho cha mjasiriamali pekee bila tozo.
Kwa upande wake mmoja wa wajasiriamali Bi Theodora Musa ambaye anatokea kikundi cha msaneza ushonaji amesema,"vitambulisho hivi nimevielewa kwani vitatusaidia saana kutokana na kuweka muda mrefu wa miaka mitatu na hivyo nawashauri wajasiriamamli wenzangu waeze kukata vitambulisho hivi kwani vitatusaidia kufanya biashara bila kusumbuliwa".