Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Bw.Dollar Rajab Kusengewakati wa kikao cha kutathmini maendeleo ya utendaji kazi wa kila idara kwa robo ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Katika kikao hicho kilichofanyika kwa siku mbili Bwana Dollar amewaagiza wakuu wa idara na vitengo kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuongeza tija na ufanisi katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwome ukusanyaji wa mapato,usimamizi wa miradi ya maendeleo,elimu,afya,kilimo na ustawi wa jamii.