WAKUU WA SHULE NA WARATIBU ELIMU KATA KUPATIWA MAFUNZO YA SHULE SALAMA ILI KUWEZA KUPUNGUZA UKATILI KWA WATOTO
Wazazi na walezi Halmashauri ya Mji wa Kasulu wametakiwa kuendelea kuToa elimu ya ukatili kwa watoto wao ili waweze kujikinga na vitendo vya kikatili wawapo shuleni na majumbani.
Hayo yalisemwa na Afisa Elimu Taaluma Bw. Jeremia Ntiboneka wakati wa mafunzo salama kwa wakuu wa shule na waratibu elimu kata na kusema,”tumetoa mafunzo haya lengo kubwa ikiwa ni kuwapa dondoo za namna ya kuenenda katika kutekeleza dhana ya shule salama na wao wakawaelekeze walimu wa malezi na unasihi katika kutekeleza majukumu yao katika kuwahudumia wananfunzi hivyo nitoe rai kwa jamii kuendelea kuwaelimisha watoto wao kuripoti matukio ya kikatili”.
Kwaupande wake Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Mji Bw. Salumu Masaga ametoa rai kwa jamii ni kuthaminiana,kuacha mila potofu na kwa kufanya hivyo wazazi watapata elimu ya unasihi na kuweza kuwasaidia watoto kuweza kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na kuweza kuwasaidia kujikinga na ukatili.
Aidha mkuu wa shule ya sekondari ya mwilamvya bw.Emmanuel Saguda alisema semina hiyo ya shule salama imemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo kwa kushirikiana na wakuu wa shule wenzake tutayatekeleza yote tuliyojifunza na tuanatarajia kwenda kuzibadilisha mada hizi kwenye utekelezaji kwa kupunguza utoro mashuleni na kuendelea kutoa elimu kwa wazazi kuwalinda watoto na kuwapa haki hasa kuwalinda na vitendo vya kikatili pamoja kwa kuwapa elimu.