• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Kasulu Town Council
Kasulu Town Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Kasulu Town Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Department
      • ELIMU SEKONDARI
      • ELIMU AWALI NA MSINGI
        • MAENDELEO YA JAMII
      • MAENDELEO YA JAMII
      • MIUNDOMBINU MAENDELEO YA MJINI NA VIJIJINI
      • HUDUMA ZA AFYA USTAWI WA JAMII NA LISHE
      • VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI
      • KILIMO MIFUGO NA UVUVI
      • MIPANGO NA URATIBU
      • UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU
    • Units
      • USIMAMIZI WA TAKA NGUMU NA USAFI WA MAZINGIRA
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • FEDHA NA UHASIBU
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA UNUNUZI
      • TEHAMA
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • NMALIASILI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
      • MALIASILI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
  • Investment opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Agriculture
  • Councillors
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Ratiba
      • Ratiba
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipango Miji Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Uchumi Elimu Afya na Maji
  • Projects
    • Proposed Projects
    • On-going-Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Brochures
    • By Law
    • Strategic Plan
    • Reports
  • Media Centre
    • Video
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

WANAFUNZI WA VYUO KASULU MJI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI UCHAGUZI, WAASWA KUTOKUTUMIWA VIBAYA NA WANASIASA

Posted on: August 21st, 2025

Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Bw. Daniel Kaloza, ameendelea na zoezi la kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi ambapo leo ametembelea vyuo vya elimu ya kati  vilivyopo mjini Kasulu. Vyuo vilivyotembelewa ni pamoja na Chuo cha Ualimu Kabanga, Chuo cha Ualimu Kasulu na Chuo cha Ufundi FDC. Ziara hiyo imefanyika kwa kushirikiana na timu ya wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya halmashauri pamoja na maafisa habari.

Katika hotuba yake, Bw. Kaloza amewasisitiza wanafunzi kuhusu umuhimu wa kujitokeza kupiga kura na kuzingatia taratibu za kisheria siku ya uchaguzi ili kulinda amani ya nchi. Ameonya vijana kutokutumiwa na wanasiasa wenye malengo ya kujinufaisha binafsi kwa kuanzisha vurugu, na badala yake amewataka kuwa mabalozi wa amani na mshikamano katika kipindi chote cha uchaguzi.

Aidha, Bw. Kaloza amebainisha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezingatia makundi maalum kwa kuyawekea mazingira rafiki ya kupiga kura. Ametolea mfano watu wasioona ambao wameandaliwa karatasi maalum za kura zenye maandiko ya nukta nundu, wafungwa watakaopiga kura wakiwa magerezani, pamoja na makundi mengine ambayo yatapewa nafasi sawa kushiriki. Amesisitiza kuwa hakuna kundi litakaloachwa nyuma katika mchakato huu wa kidemokrasia.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi Masalu Chama kutoka Chuo cha Ualimu Kabanga ameeleza kuwa wametiwa moyo na elimu waliyoipokea na wamejipanga kuwapuuza wanasiasa watakaokuja kwa lengo la kuwatumia. Aidha, aliongeza kuwa elimu hiyo imewapa hamasa kubwa ya kushiriki uchaguzi kwa amani na kwa kuzingatia misingi ya demokrasia.

Elimu ya mpiga kura inaendelea kutolewa pia katika kata mbalimbali za Halmashauri ya Mji Kasulu ambapo wananchi wanapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata uelewa wa kina kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi. Hatua hii inalenga kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu na kwa amani katika zoezi la kidemokrasia linaloendelea nchini.

"Kura yako Haki yako Jitokeze Kupiga Kura"

Announcements

  • NAFASI ZA KAZI March 19, 2025
  • TANGAZO LA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA April 30, 2025
  • TANGAZO LA KAZI July 01, 2025
  • View All

Latest News

  • Mapato ya Ndani Yaleta Matunda – Wananchi Kumnyika Wafaidika na Soko la Kisasa

    August 25, 2025
  • WANAFUNZI WA VYUO KASULU MJI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI UCHAGUZI, WAASWA KUTOKUTUMIWA VIBAYA NA WANASIASA

    August 21, 2025
  • WANAFUNZI WA VYUO KASULU MJI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI UCHAGUZI, WAASWA KUTOKUTUMIWA VIBAYA NA WANASIASA

    August 21, 2025
  • WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI WAAPISHWA RASMI – WAASWA KULINDA UADILIFU NA AMANI

    August 04, 2025
  • View All

Video

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
More Videos

Quick Links

  • News

Related Links

  • TAMISEMI
  • Ega
  • Utumishi
  • Kigoma Region

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Test

Copyright ©2017 Kasulu Town Council. All rights reserved.