WANANCHI MJINI KASULU WASISITIZWA KUZINGATIA USAFI WA MAZINGIRA ILI KUJIEPUSHA NA MAAMBUKIZI YA MAGONNWA YA MILIPUKO
Kufuatiwa baadhi ya maeneo nchini kuripotiwa kuwa na ugonjwa wa mlipuko wa Kipindupindu wananchi wa Halmashauri ya Mji Kasulu washauriwa kuchukua tahadhari mapema kwa kufanya usafi wa mazingira yanayoowazunguka ili kuepukana na ugonjwa huo.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji kasulu mara baada ya kufanya usafi wa mwisho wa mwezi katika mahojiano na kitengo cha mawasiliano serikalini mwishoni mwa mwezi Januari ameendelea kusisitiza wananchi kufanya usafi katika maeneo yao ili kuweka mazingira safi na kuepukana na magonjwa.
Amesisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kufanya usafi katika maeneo yao bila yakushuurutishwa na kutunza taka katika vifaa malumu na utupa mahali sahihi.
“Katika kipindi hiki cha mvua wananchi wakate nyasi kwenye maeneo yao na kwa wafanya biashara kuhifadhi taka katika vitunzia taka kusubiri magari ya taka na pia nitoe rai kwa wale wananchi wanaotupa taka hovyo hasa kwenye mifereji na wale wanaofungulia chemba wakati huu wa mvua waache kufanya hivyo kwani wanaweza kuleta hatari kwa afya zao ukizingatia kipindi hiki baadhi ya maeneo kuripotiwa kuwa na kipindupindu hata hivyo kwetu sisi hatujapata taarifa ya ugonjwa huo.
Ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kutunza manzingira na kuchemsha maji ya kunywa pia kula chakula kilichoandaliwa vizuri pamoja hifadhi mazingira ya choo.
Aidha amesema wananchi wanatakiwa kuzingatia siku za usafi ambao kwa halmashauri alhamisi kila week inatumika kufanya usafi wa mazingira na jumamosi ya mwisho wa mwezi hivyo kutumia muda huo kufanya usafi kama inavyotakiwa.