Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bw.Thobias Andengenye amewataka wananchi wa kata ya murufyiti iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kasulu kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa CHF ili kuwasaidia kwa urahisi katika matibabu. Aliyasema hayo 19,Augosti 2021.
Aliyasema hayo 19,Augosti 2021 katika ziara yake ya siku moja katika kata hiyo ambapo aliwataka wananchi kupiga vita ukatili wa kijinsia,kinjinsia na kingono unaofanywa kwa wanawake na watoto na kutoa wito kwa wananchi kutoa ushahidi mahakani pindi kesi za kikatili zinapotokea ili haki itendeke.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bw.Nurfus Aziz amesema kuwa ilikuendelea kuboresha maendeleo wanakijiji wameweza kuboresha barabara za mitaa,kufyatua matofari na kujenga soko kwa nguvu zao wenyewe hii ikiwa ni moja ya kuisaida serikaliya Tanzania kuhimiza maendeleo katika vijiji,wilaya,mikoa na nchi kwa ujumla.
Aidha baadhi ya wananchi wa kata hiyo ameishukuru serikali kwa kuunga juhudi za kimaendeleo za wananchi na kuiomba serikali kuboresha zaidi huduma za umeme,kilimo kwa zao la michikichi na afya kwa kuongeza wataalamu wa afya na kuboresha huduma za maabara.
Mwisho Andengenye amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa,kunawa maji tiririka na kutumia vitakasa mkono pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyokuwa na lazim