WANANCHI WTAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUFANYA USAFI
Viongozi n wananchi wa halashauri ya kasulu wamesisitizwa kuweka mikakati katika utunzaji wa mazingira
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa kigoma mheshimiwa thobias andengenye wakati wa maadhimisho ya uzinduzi wa usafi wa mazingira kitaifa leo januari 25 2023 na kusema,”viongozi wote wekeni mikakati ya kutunza mazingira pamoja na upandaji miti ili kuweza kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita”
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuukazi,vijana,ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa kaulu mjini Profesa joyce lazaro ndalichako amewasisitiza wananchi umuhimu wa kupanda miti na usafi wa mazingira ili kuweza kuepukana na janga laukosefu wa mvua na kupoteza vyanzo vya maji.
Kwa upande wao wananchi wa mji wa kasulu wametoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana kwa pamoja kufanya usafi na kuahidi ushirikiano kwa viongozi wao na paia zoezi hili litakuwa endelevu ili kufanya mji wa kasulu kuwa safi.
Ikiwa ni siku ya uzinduzi wa safi wa mazingira kwa taifa mkoa wa kigoma wananchi wamesisitizwa kuituma kauli mbiu hii “UTUNZAJI WA MAZINGIRA SALAMA KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU” ambayo ni ktika utekelezaji wa maagizo ya ofisi ya makamu wa rais dr.philpo isidory mpango