WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI ILI KUEPUKA UKAME
Wananchi wa kata ya heru ju wametakiwa kutunza vyanzo vya maji kwa kwa kupunguza kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya kasulu kanal isack mwakisu wakati akiongoza zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji cha mto chogona kusema”vyanzo hivi vikiendelea kuntunzwa na kuhifadhiwa vitaongeza mvua nyingi na kutunza mazingira ili kutosababisha hali ya ukame”
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya mji kasulu bwana dollar rajab kusenge ameeendelea kuwasisitiza wananchi wa mji kasulu kuendelea kutunza mazingira na kusema kuwa wameweka alama za mipaka ili kuwaonyesha ni wapi shughuli za kibinadamu zinatakiwa kuishia na hivyo kuwataka kutokuvuja sheria ili hatua kali zisichukuliwe dhidi yao.
Nao baadhi ya wananchi ambao wanajishughulisha na utunzaji wa mazingira wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya athari za kutokutunza na kuhifadhi mazingira hii tawafanya wananchi wengi kuwa wazalendo na kuendelea kuepuka kufanya shyghuli zinazochangia uharibifu wa mazingira.