WATAALAM MKOANI KIGOMA WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI KWA WELEDI ILI IWEZE KUKAILIKA KWA WAKATI
Na.
Mwandishi Wetu
Mkurugenzi idara ya usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI bw.Vicent Kayombo amewataka wataalam wa Mkoa wa Kigoma kusimamia utekelezaji wa miradi ya serikali kwa umakini na weledi.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na wadhibiti ubora , maafisa Elimu kata na wakuu wa shule za msingi na sekondari baada ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya serikali inayotekelezwa kupitia BOOST na serikali kuu na kusema,"nimepita kukagua miradi yenu kwa asilimia kubwa mmejitahidi katika kusimamia vizuri miradi hii ya madarasa kwa baadhi ya maeneo imekamilika na pengine haijakamilika ila nawaomba muhakikishe mnasimamia kikamilifu miradi hii ambayo tunaijenga kutokana na lipa kwa matokeo na tukimaliza kwa wakati tutakuwa tumekidhi vigezo vya kupata fedha nyingine za kuwapelekea wenye uhitaji".
Aidha Kayombo ameendelea kusema "sisi kama Ofisi ya Rais TAMISEMI hatuko tayari na hatutokubaliana na yeyote atakayecheza na fedha za serikali hivyo viongozi tuongeze umakini katika usimamizi wa miradi ya serikali ili ikamilike kwa wakati hasa kwa kuzingatia ubora wa vifaa vinavyotumika".
Kwaupande wake Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma Bi Paulina Ndigeza amewasisitiza wataalamu waliohudhuria kikao hicho na kusema,"niwaombe tukayafanyie na kuyatekeleza maagizo yote tuliyopatiw ikiwa ni pamoja na kushirikiana na kuhakikisha tunapandisha ufaulu wa mitihani kwa shule za msingi".
Lengo la ziara ya hiyo ilikuwa ni kukagua taaluma na miradi ya maendeleo.