WATAALAMU WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO
Wataalam wa Utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na msingi "BOOST' wametakiwa kutekeleza majukumu yao ili kupata matokeo chanya katika utekelezaji wa mradi huo mara baada ya kupata ujuzi mpya wa kujengewa uwezo na kuhakikisha wanafanya maboresho makubwa katika mfumo wa elimu Nchini
Ameyasema hayo Bi. Paulini Ndigeza alipokua akifungua mafunzo elekezi kwaajili ya kuwajengea uwezo Wataalamu Wa Utekelezaji Wa Mradi huo kwa kanda ya magharibi Kanda ya Magharibi yaliyofanyika Katika Chuo Cha Ualimu Kasulu Mkoani Kigoma.
"Tutumie nafasi hii kujifunza kwa bidii na tuhakikishe tunaelewa dhamira ya mradi huu kwa kuwa malengo ya serikali na wahisani ni kuhakikisha tunafanya maboresho makubwa katika mfumo wa Elimu nchini ikiwemo kuongeza udahili wa elimu awali pamoja na kujenga mazingira rafiki ya ujifunzaji na ufundishaji" amesema Ndigeza
Aidha amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha Fedha na kuidhinisha ujenzi wa Miundimbinu ya Elimu pamoja na kuwezesha utekelezaji wa kazi mbalimbali za kielimu nchini.
Kwa upande wake Mwezeshaji Wa Mafunzo hayo Bi. Joyce Mushi kutoka OR-TAMISEMI, amesema mradi huo wa BOOST unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, unathamani ya shilingi Tril. 1.5 ambazo ni ufadhili wa benki ya dunia ukiwa una lengo la kuzifikia shule 6000 na kuwafikia zaidi ya watoto milion 12 nchinii.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanaratibiwa na kutekelezwa na Wizara ya OR-TAMISEMI, wizara ya Elimu na Sayansi na teknolojia pamoja na Wizara ya Fedha ambapo washiriki wanajengewa uwezo katika afua za uboreshaji wa miundombinu, uwekaji mazingira salama ya ufundishaji na ujifunzaji, kuongeza udahili wa wanafunzi wa elimu awali, uboreshaji mazingira ya kielimu, utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu kazini, kuwezesha upatikanaji wa rasilimali za utoaji huduma katika Halmashauri
Timu za utekelezaji wa mafunzo hayo, zinaundwa na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Elimu Msingi, Manunuzi, Maendeleo Ya Jamii, Uthibiti Ubora wa Elimu Walimu ngazi ya Shule za Msingi Wahandisi, Maafisa Habari pamoja na Mratibu Ngazi Ya Mkoa