WATENDAJI WA KATA KUMI NA TANO ZA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WANASIMAMIA NA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Watendaji wa kata za Kasulu mjini wameombwa kuhamasisha wananchi katika kata zao ili waweze kushirikik kikamilifu katika zoezi zima la sensa ifikapo tarehe 23 Agosti mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Bw.Dollar R. Kusenge katika kikao kilichofanyika leo tarehe 10 mwezi wa 8 na watendaji wote wa kata za Kasulu mjini na kusema’’watendaji mnatakiwa kuandaa mpango mkakati ,kusoma ilani ya chamana kuandaa namna ya kuhamasisha utekelezaji wa zoezi la sensa.
Dollar ameendelea kuwasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanatolea maelezo fedha na miradi inayopokelewa kwenye kata zao kwa wananchi hasa kwenye vikao vya kata,kushiriki na kusimamia kwa ufasaha matukio yayayofanyika katika kila kata na urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmasahuri kwa vijana ,wanawake na wenye ulemavu.
Aidha watendaji hao wametakiwa kuhakikisha wanakutana na makundi maalumu kwenye kila kata ili kuweza kuwahamasisha kushiriki zoezi la sensa na makazi litakalofanyika agost 23 mwaka huu
Kikao hicho kililenga kutoa maelekezo kwa watendaji wa kata juu ya usimamizi wa zoezi la sensa kwa ajili ya kupata takwimu za kidemografia za watu na makazi kikamilifu katika mji wa Kasulu.